The House of Favourite Newspapers

Snura Adaiwa Kupangiwa Nyumba na Mwarabu

Muonekano wa nyumba ambayo inadaiwa Snura kapangiwa na mwarabu.

Na HAMIDA HASSAN| GLADNESS MALLYA| IJUMAA WIKIENDA| UBUYU ULIONYOOKA

DAR ES SALAAM: Ubuyu wa mjini! Staa wa muziki na sinema za Kibongo, Snura Mushi anadaiwa kupangiwa nyumba na mwanaume wa Kiarabu maeneo ya Tabata, Dar aliyeamua kumuhamisha Mwananyamala kwa sababu hakuyapenda mazingira aliyokuwa akiishi mwanamama huyo awali.

Snura Mushi.

TUJIUNGE NA MTOA UBUYU WETU

Kwa mujibu wa mtoa ubuyu wetu, Snura siku hizi ametulizwa huko Tabata ndiyo maana hasikiki kivile kwani mbali na kupangishiwa mjengo huo mzima, pia amenunuliwa mkoko wa kutembelea.

SIKIA UBUYU UKIMUNG’UNYWA

“Hivi Wikienda mnajua kilichomfi cha Snura siku hizi mpaka hasikiki sana? Bidada ametulizwa na mwanaume wa Kiarabu ambaye amempangia mjengo wa maana.

“Nasikia huyo jamaa ndiye aliyemfanyia mpango wa ile safari ya Oman aliyoifanya kipindi kile. Unaambiwa Snura anaishi kwenye mjengo wa maana Tabata wenye bonge la uwanja wa kujiachia,” alinyetisha mtoa ubuyu wetu.

WANAUBUYU KAZINI Kama ilivyo ada ya kuchimba, wanaubuyu wetu walizama kazini na kuanza kunusanusa ili kubaini nyumba hiyo. Wikienda lilianza kuichambua Tabata kupeleleza nyumba hiyo hadi lilipofi ka na kufanya yake ambapo walipiga mapichapicha ya haraka ili kuupata ushahidi kama picha zinavyoonesha.

SNURA ATOKEA MLANGO WA NYUMA

Baada ya picha kadhaa za mazingira ya nyumba hiyo, Snura aliwashtukia wanaubuyu wetu ambapo alitokea mlango wa nyuma kisha akawavaa. Snura alianza kuwahoji wanaubuyu wetu sababu za kufi ka nyumbani kwake bila taarifa ndipo walimuomba atulie na kuwasikiliza.

Wikienda: Snura mambo vipi? Mbona kimya sana kimuziki? Au ndiyo mambo ya ubuyu unaosemwa?

Snura: Yapi tena? Mimi mbona nipo najiandaa kutoa kazi? Siyo kila siku kusikika bila mpango. Mimi huwa nasikika kwa kazi ninayoitoa ninyi subirini mtanisikia.

Wikienda: Hata hivyo, tuna ubuyu hapa kuwa nyumba hii umepangishiwa na mwanaume wa Kiarabu ambaye amekuhamisha Mwananyamala kwa sababu alikuwa hapapendi, unalizungumziaje hilo?

Snura: Hahahahaha, mmenichekesha kweli, watu wanajua kuongea sana, mimi nimehama nyumba kwa sababu ya mtoto. Shule anayosoma mwanangu ipo huku Tabata. Mwananyamala ilikuwa ni mbali sana. Mwanangu alikuwa anachoka sana. Hayo mengine ya mwanaume wa Kiarabu ndiyo kwanza nayasikia kwenu.

Wikienda: Nasikia amekununulia na gari la kutembelea maana tunaliona hapa, tunasikia ana mpango wa kukupiga stop kuimba, je, ni kweli?

Snura: Gari nimenunua mwenyewe kwa jasho langu nikimaanisha kazi yangu, huyo Mwarabu mnayemkazania kama yupo hakuna la kufi cha kwani mwisho wa yote atajulikana tu na ataonekana, lakini nahisi labda wanayemzungumzia ni baba mtoto wangu, hahaha…

KUTOKA MEZA YA MHARIRI Ubuyu ndiyo huo na ukweli umejulikana, wanaubuyu bado wapo kazini kumnasa mwanaume huyo na mambo yote yatakuwa hadharani.

 

Comments are closed.