The House of Favourite Newspapers

Mwanaheri; Soko la Filamu Lipo! (+ video)

0
Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ (kulia) akiwa na mdau wa filamu Bongo.

Na GLADNESS MALLYA| RISASI MCHANGANYIKO| ZA MOTOMOTO

WAKATI wakongwe wa filamu Tanzania wakilia usiku na mchana juu ya kufa kwa soko la kazi zao, msanii kutoka tasnia hiyo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ ameibuka na kupinga madai hayo, akisema wanaodai hivyo ni watu ambao wakati wao umeshapita.

Akizungumza na Za Motomoto News, Mwanaheri alisema siyo kweli kwamba soko limekufa, isipokuwa wasanii ambao hawapati kazi kwa sasa ni wale ambao wakati wao wa kuvuma umepita kwani kazi za fi lamu zinaenda na muda ambao mtu hawezi kulazimisha.

“Filamu haijafa jamani ila soko tu ndiyo limeshuka kwa sababu bado tunafanya fi lamu na zinafanya vizuri tu, wanaosema sanaa ya fi lamu imekufa ni waongo, na niseme tu muda wao umepita huu ni wakati wa wengine kufanya kazi,” alisema Mwanaheri.

Nimekuwekea Hapa Video ya Steve Akieleze Sekeseke la Filamu Tanzania.

Leave A Reply