The House of Favourite Newspapers

TUKIO LA MO DEWJI, IGP SIRRO AWATAHADHARISHA LEMA, ZITTO – VIDEO

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, amesema Jeshi la Polisi linaumizwa na kitendo cha baadhi ya Watanzania na wanasaiasa kulichafua jeshi hilo mitandaoni kwa uchunguzi wake kufuatia sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye amepatikana usiku wa kuamkia leo baada ya kutupwa katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam.

 

Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari, jijini Dar es Salaam jijini wakati akitoa ufafanuzi baada ya ya Mo kupatikana huku akiwataka wanasiasa (bila kuwataja majina) na baadhi ya Watanzania kutumia mitandao ya kijamii kubeza kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo katika kushughulikia matukio mbalimbali ya ya uhalifu.

 

“Kuna kikundi cha watu wachache wanajaribu kujenga uadui na Jeshi la Polisi, sijui wanatumwa na nani, polisi tukifanya kazi zetu wanaingilia, kama wana agenda yao ya siri wasije wakalaumu, katika matukio mengi wao ndiyo wanajifanya wanatuelekeza wanajua kila kitu.

 

“Mambo ya mitandao yanatuumiza sana sisi ambao hatulali kufanya upelelezi huu, kuna mtu anakaa muda wote gesti, anakunywa wine anakunywa bia, yeye anazunguka mitandaoni tu, anatufundisha kila kitu, criminal investigation anajifanya anajua kila kitu, mimi ninawaambia waache mara moja,” alisema Sirro.

 

Jana baada ya IGP Sirro kuonyesha picha iliyopigwa kutoka kwenye CCTV camera ikionyesha gari lililotumika kumteka Mo, wabunge Zitto Kabwe, Goodbless Lema na baadhi ya Wananchi waliandika mitandaoni wakipinga kuwa haikuwa picha iliyopigwa kwa CCTV jambo lililoibua mijadala mitandaoni kisha Lema akasema angezungumza na wanahabari leo lakini ameahirisha.

 

VIDEO: IGP SIRRO AKIFUNGUKA

Comments are closed.