The House of Favourite Newspapers

Kimenuka! Alikiba Amcharukia Diamond: “Unikome, Nitakuvua Nguo”

IKIWA ni saachache baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutangaza kuwa Meneja wake, Babu Tale ameshafanya mawasiliano na Menejimenti ya msanii mwenzake, Alikiba kuhusu ushiriki wake wa kwenye tamasha la Wasafi Festival litakalofanyika Novemba 9, jijini Dar es Salaam, Alikiba naye amemjibu Diamond tena kwa ghadhabu.

 

Kiba kupitia ukurasa wake wa Instagram kumjibu Diamond kwa kuandika, “Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME) Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz,“.

 

Hii ni mara ya pili kwa Alikiba kukataa kutumbuiza kwenye tamasha hilo la Wasafi Festival, alifanya hivyo pia mwaka jana ambapo alisema yupo tayari kutoa udhamini kupitia kinywaji chake cha Mo faya badala ya kufanya shoo.

 

Leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Diamond wakati akizungumzia tamasha hilo litakalofanyika Novemba 9, 2019  jijini Dar es Salaam alisema ana imani Harmonize atashiriki na kwamba amepeleka mwaliko kwa uongozi wa Ali Kiba, ili msanii huyo naye ashiriki tamasha hilo.

“Wenzetu Nigeria ndio maana wanaendelea kwenye muziki kwani kunapokuwa na matamasha kama haya wanaweka tofauti zao pembeni, kumkuta jukwaa moja Wizkid na Davido ambao walikuwa na bifu kwao ni jambo la kawaida.”

“Kwa nini tung’ang’anie bifu hata sehemu ambayo ni ya kutengeneza pesa na kutuleta Watanzania pamoja,” amesema Diamond katika mkutano wake huo na waandishi wa habari.

Harmonize kwa upande wake alipoulizwa alijibu;  “achana na hayo mambo ya Diamond, tuongee mambo mengine.”

 

Comments are closed.