The House of Favourite Newspapers

Aliyejifanya Ofisa TAKUKURU Anaswa, Afikishwa Kortini

0

Mfanyabiashara, Edson Beanga Mkazi wa Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujifanya kuwa Ofisa wa TAKUKURU kinyume cha sheria.

 

Mshtakiwa Beanga amefikishwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon akimsomea mashtaka yake amedai, Desemba 11 hadi 15, mwaka huu jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alijifanya kuwa ni afisa wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) na kujitambulisha kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Juma said Tandu ambaye ni mchunguzi wa Takukuru jambo ambalo lilikuwa siyo kweli.

 

Shtaka la pili ni kughushi, inadaiwa Agosti 4, mwaka 2018 jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alitengeneza nyaraka ya uongo ambayo ilikuwa ni fomu iliyokuwa ikionesha kuwa ilitolewa na Takukuru jambo ambalo siyo kweli.

Shtaka la tatu ni kughushi, ambapo inadaiwa Agosti 4, mwaka 2018 katika jiji la Dar-es-Salaam mshtakiwa alitengeneza nyaraka ya uongo ambacho kilikuwa ni kitambulisho kikionesha kimetoka NEMC ambapo kilionesha ni cha mtu aitwaye Boniface Mlema, kwamba kilitolewa na NEMC kumbe ni uongo.

 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Wakili wa jamhuri alidai upelelezi bado aujakamilika na Hakimu Chaungu ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 14, 2021 ambapo itatajwa na mshtakiwa amepelekwa rumande.

Leave A Reply