The House of Favourite Newspapers

Azam Walia Majeruhi Kuwafelisha

0

Omary Mdose | CHAMPIONI| Dar es Salaam

IMEELEZWA kuwa, kitendo cha timu ya Azam FC kukumbwa na wachezaji wengi majeruhi wa kikosi chao cha kwanza, ndicho kimeifelisha timu hiyo kwenye mbio zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Azam ambayo kwa sasa haipo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo, inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 45 huku ikiachwa pointi 13 na vinara Simba na 11 dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili, Yanga.

Ofi sa habari wa timu hiyo, Jaff ar Idd, amesema: “Majeruhi wengi hasa wa kikosi cha kwanza ndio wanaosababisha matokeo mabaya kwa timu yetu na kutufanya tushindwe kufi kia malengo.

“Kwa sasa tuna wachezaji watano majeruhi ambao ni Stephen Kingue, Yacub Mohammed, Aggrey Morris, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na John Bocco, utaona hao ni wachezaji wetu muhimu na tumewakosa katika mechi kadhaa muhimu ikiwemo dhidi ya Mtibwa tuliyotoka suluhu.”

Leave A Reply