The House of Favourite Newspapers

Baba Zuchu: Damu Nzito Kuliko Maji, Nafurahi Kumuona Zuchu

0

Siku zote waswahili husema damu nzito kuliko maji! ndivyo ilivyotokea kwa baba wa msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othuman ‘Zuchu’, Othuman Soud ambaye huko nyuma kulikuwa na madai mazito kuwa baba huyo hakuwa na mawasiliano mazuri na mtoto wake.

 

Baba wa msanii huyo ambaye makazi yake ni Makadara – Visiwani Zanzibar, amefunguka kuwa kila siku anamuombea mtoto wake huyo azidi kuwa bora kwa maana mafanikio ya Zuchu, ni mafanikio yake pia.

 

Mbali na hilo pia alizungumza kuhusiana na muziki anaofanya mwanaye huyo na mambo mbalimbali alipokuwa akizungumza na AMANI kama ifuatavyo:

 

AMANI: Habari za siku baba! pole na kuumwa.

 

Baba Zuchu: Asante sana. Sasa hivi afadhali kidogo naendelea vizuri sana angalau naweza kutembea mwanzo nilikuwa sitembei kabisa wala kukaa, maana nilipooza kuanzia kiunoni kwenda chini.

 

AMANI: Pole sana, vipi Zuchu anakuja kukuona?

Baba Zuchu: Ndio, juzi tu katoka kuniona hapa… maana sasa kila mara anakuja kuniona.

 

AMANI: Unajisikiaje ukiona sasa na mwanao, mko vizuri na anakuja kukuona hivi unaumwa?

 

Baba Zuchu: Najisikia vizuri sana, nafurahi mno, maana yule ni mtoto wangu… nampenda.

 

AMANI: Unajisikiaje kuhusiana na kazi yake ya muziki anayofanya sasa hasa ikizingatiwa ni msanii bora wa kike. Baba

 

Zuchu: Najisikia vizuri sana, huwa naamka usiku na kumuombea siku zote ili atazidi kuwa bora zaidi.

 

AMANI: Unaye mtoto mwingine ambaye anaimba au amefuata nyayo kama ilivyo kwa Zuchu?

 

Baba Zuchu: Hakuna mtoto mwingine aliyefuata nyayo zangu zaidi ya kwake na ninamshukuru Mungu sana kwa ajili yake.

 

AMANI: Umekuwa baba wa tofauti sana, maana watu wengi hawakufahamu kwanini?

 

Baba Zuchu: Mimi kwa kweli tangu zamani sipendi mambo ya mtandao na sijui lolote kuhusu mtandao, hivyo siwezi kuja kuonekana hovyo hovyo mitandaoni.

 

AMANI: Kuhusu ugonjwa umeshapata ufumbuzi?

 

Baba Zuchu: Nimeshapata na ndio nafanya matibabu na sasa ni afadhali sana, hata naweza kutembea maana mwanzo hata kukaa nilikuwa siwezi kabisa.

 

AMANI: Haya baba ugua pole baba. Baba Zuchu: Asante sana, karibu tena.

MAKALA: IMELDA MTEMA, ZANZIBAR

Leave A Reply