The House of Favourite Newspapers

Baby Madaha: Sina Marafiki Wabwia Unga

Baby Madaha

STORI: GLADNESS MALYA | RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amefunguka kuwa licha ya mastaa wengi kuwa na wasiwasi wa kutajwa majina yao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kama wengine, yeye hana shaka kwani hatumii na wala hana marafiki wanaojihusisha na ishu hiyo.

Baby Madaha

Akipiga stori na Risasi Vibes,  Baby Madaha alisema hana wasiwasi wa kuitwa kwa sababu hajawahi kutumia na hana kampani ya wanaotumia kwa sababu akianza urafiki na mtu huwa anamfanyia uchunguzi kwanza na akiona haelekei, anampotezea.

Baby Madaha

“Sijawahi kutumia unga wala sina kampani ya wanaotumia au kusafirisha, maana marafiki zangu wote na watu wa karibu kabla sijaanza ukaribu nao huwa nawachunguza kwanza, hivyo najiamini na Watanzania wanatakiwa watambue kuwa Makonda hajakurupuka, vita ndiyo imeanza na mifano hai itatokea kwetu sisi wasanii,” alisema Baby Madaha.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.