The House of Favourite Newspapers

Bella Kuwa Refa Gigy Money vs Pam D, Dar Live

0

 

King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.

WAKATI zikiwa zimesalia siku mbili kufikia Mei 6, King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuwa refa katika mpambano wa nani mkali wa kuimba kati ya Pamela Daffa ‘Pam D’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Gift Stanford ‘Gigy Money’.

Mwandishi Wetu | Championi Jumatano | Habari

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, shoo nzima inatarajiwa kuanza saa mbili za usiku ambapo Bella pamoja na bendi yake ya Malaika, wataanza kwa kutoa burudani ya nguvu kwa kupiga nyimbo zao zote kali.

“Mashabiki wajipange na wajiandae kwa shoo ambayo tangu mwaka uanze Bella hajawahi fanya. Hiyo ni fursa kubwa mashabiki wote wanaoizunguka Dar Live na Dar es Salaam kwa ujumla. “Usiku huo zitapigwa nyimbo zote kuanzia Yako Wapi Mapenzi, Nashindwa, Nani Kama Mama, Msaliti, Nishike na nyingine kibao,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 7,000 tu.

Pamela Daffa ‘Pam D’

Naye Bella alitia neno kuwa kwa mara ya kwanza tangu aanze muziki atakuwa refa katika mpambano wa Gigy Money na Pam D ambapo bingwa atapata tiketi moja kwa moja ya kutengeneza naye kolabo na video.

“Wote wanajulikana kama ni wasanii ambao ni wazuri. Kila mmoja ana jina hivyo ni wakati wa wewe shabiki kuamua nani mnaona anafaa nifanye naye kolabo. Usiku huo mshindi nitamvalisha ‘crown’ maalum,” alimaliza Bella.

Leave A Reply