The House of Favourite Newspapers

Boris Johnson na Carrie Wapata Mtoto Mwingine Ndani ya Miezi 20

0

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na mkewe Carrie Johnson wametangaza kuzaliwa kwa binti, mtoto wao wa pili tangu awe waziri mkuu. CarrieĀ ameijifungua mtoto huyo katika Hospitali ya London mapema leo Alhamisi, na Johnson alikuwa huko muda wote.

 

Msemaji wa wanandoa hao amesema; “Mama na mtoto wanaendelea vizuri sana” na alishukuru timu ya NHS kwa utunzaji na msaada wao. Wawili hao waliofunga ndoa Mei mwaka huu, pia wana mtoto wa kiume, Wilfred, ambaye alizaliwa Aprili mwaka jana 2020 (hii ni miezi 20 pekee tangu kuzaliwa kwa Wilfred).

 

Kuzaliwa kwa Wilfred kulikuja wiki chache baada ya Johnson kuruhusiwa kutoka katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kufuatia matibabu ya virusi vya corona.

 

Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer alituma pongezi zake kwa kuzaliwa kwa binti wa wanandoa hao, na kuongeza: “Tunaitakia familia yako afya na furaha.”

 

Habari hizo zinakuja katika wiki yenye misukosuko kwa waziri mkuu huyo, huku kukiwa na msukosuko wa umma na wa kisiasa juu ya vizuizi vipya vya Covid-19.

Leave A Reply