Breaking: Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa Bin Zayed Afariki

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan.

 

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki, shirika la habari la Imarati WAM limeripoti muda mfupi uliopita na kusema amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

 

“Wizara ya Masuala ya Rais ilitangaza kuwa kutakuwa na siku 40 za maombolezo rasmi na bendera nusu mlingoti na siku tatu kufungwa kwa Wizara na Mashirika rasmi katika ngazi ya shirikisho na Serikali za mitaa na sekta ya kibinafsi” taarifa imeeleza.

 

Sheikh Khalifa ambaye amekuwa akiugua kwa miaka kadhaa kulikosababisha kwa muda mrefu aache kujihusisha na shughuli za kila siku alimuachia mikoba kaka yake ambaye ni Mwanamfalme wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed ambaye ndiye ameonekana kama Mtawala kwa muda huo.

 

Sheikh Khalifa ambaye ni nadra kuonekana kwenye picha rasmi au kwenye hafla za umma kwa miaka mingi, alimrithi Baba yake na Mwanzilishi wa UAE Sheikh Zayed mnamo mwaka 2004, alipata kiharusi muongo mmoja baadaye na kumweka mbali na Watu tangu wakati huo.

RAIS SAMIA ANASHIRIKI MAADHIMSHO YA MIAKA 10 YA MUUNGANO WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU…3403
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment