The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Sakata la Kikokotoo Kazi Ipo! Bulaya Amtaka JPM Awatumbue Hawa – VIDEO

Waziri Kivuli ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Mh Ester Bulaya akizungumza na waandishi (hawapo pichani).

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaka suala la kikokotoo liwasilishwe bungeni na lijadiliwe kwa hati ya dharura ili iwe sheria itakayomnufaisha kila mstaafu.

 

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Makao makuu ya Chama hicho Waziri Kivuli ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Mh Ester Bulaya amesema pamoja na Rais wa Tanzania Dr John Magufuli kurudisha kikokotoo cha awali lakini bado haijawa sheria rasmi hali inayosababisha ubaguzi wa mafao kwa wastaafu.

“Baada ya kauli ya Rais Magufuli kuhusu kikokotoo cha wastaafu kuna mambo ya muhimu ya kufanywa, Rais ametoa huduma ya kwanza, tiba ni kurudisha sheria Bungeni kwa hati ya dharura ili haya mambo yawe kisheria yaweze kutekelezeka,” amesema Bulaya.

 

Aidha, Bulaya amesema anashangaa Rais kumtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa SSRA na kumuacha Waziri Mwenye dhamana ya Utumishi akiwa ofisini.

“Rais amfurushe kazini Waziri Mhagama au Waziri mwenyewe ajiuzulu sababu yeye ndie alietunga hizi kanuni na alizipigia debe Bungeni. Morali kazini zimeshuka sababu ya mtu mmoja halafu bado yupo ofisini is not fair, Dada yangu namheshimu ila anapaswa kuwajibika ktk hili sina chuki nae.

 

“Viongozi tuwe na utaratibu wa kukiri tunapokosea, nyie mnajua mchakato wa sheria unaanzia kwenye Baraza la Mawaziri na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ni Rais, alisaini hii sheria,” amesema Bulaya.

VIDEO: MSIKIE BULAYA AKIDUNGUKA HAPA

Comments are closed.