The House of Favourite Newspapers

Buchosa: Shigongo Awatahadharisha Watakaotafuna Fedha za Uviko 19

0

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo amewatahadharisha watendaji wa Serikali kutothubutu kula fedha za Uviko 19 zinazojenga vyumba vya madarasa jimboni humo.

 

Kauli hiyo ameitoa jana Novemba 17, mwaka huu katika Kijiji cha Kalebezo mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondari Kalebezo.

 

Shigongo amesema Mheshimiwa Rais anahangaika kutafuta fedha huku na kule ili kuwasaidia wananchi wake harafu atokee mtu mwingine kufuja fedha hizo lazima atawajibishwa.

 

Jimbo la Buchosa kwa maana ya Halmashauri ya Buchosa inajenga vyumba vya madarasa 142 sawa Sh2.5bilioni zilizotolewa na Serikali kujenga vyumba hivyo.

 

“Ninawaomba watumishi wa Serikali kusimamia vema ujenzi wa vyumba hivi na Serikali imetoa siku 45 pekeee viwe vimekalika na hakuna kisingizio chochote kwa kuwa fedha zipo,” amesema Shigongo.

 

Mmoja wa wananchi wa kata ya Kalebezo, George Safari amewataka madiwani na watendaji wa chama kufuatia na kusimamia ujenzi huo lengo ni kuhakikisha majengo hayo yanajengwa kwa ubora.

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Paul Malala amesema wamejipanga na timu yake kusimamia vema majengo hayo na yatakamika kwa wakati licha ya kuwepo changamoto ya upatikanaji wa sementia kutokana na nchi nzima kuwa ujenzi wa vyumba hivyo.

Mwandishi wetu

 

Leave A Reply