The House of Favourite Newspapers

Bunge la Marekani Lasafisha Njia Kumshtaki Trump

0

BARAZA  la Wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump kwenda katika Baraza la Seneti ikiwa ni hatua ambayo inaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani.

 

Hatua hiyo imekuja katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, tangu wabunge wa baraza hilo kumkuta Trump na hatia  ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za Bunge kuchunguza vitendo vyake.

Wabunge wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha azimia hilo kwa kura 228 dhidi ya 193. Huku Spika Nancy Pelosi akisaini uamuzi huo sambamba na timu ya wabunge wa Democratic ambao wataendesha mashtaka ya kesi hiyo inayomkabili Rais Trump.

 

Mameneja wameteuliwa leo na spika kwa ajili ya kuendesha mashtaka kutokana na kupeleka kitu ambacho kimepitishwa. maseneta kama wazee wa baraza na baadaye kupiga kura.

 

Baraza hilo  ambalo linadhibitiwa na chama cha upinzani cha Democrats, linataka  Trump aondolewe madarakani.

 

Hata hivyo Baraza la Seneti ambalo linadhibitiwa na chama tawala kinachoongozwa na Trump, kitaamua aidha kumtia hatiani na kumuondoa madarakani. Jambo ambalo halitarajiwi.

 

Katika mkutano na wanahabari kabla ya kutia saini hati, Pelosi alisema: ”Leo tutaweka historia tutakapopeleka hati za mashtaka dhidi ya rais wa Marekani kwa vitendo vyake vya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia majukumu ya bunge kushughulikia suala hilo”.

 

Hati hizo kisha zikapelekwa kwenye Baraza la Seneti, ambapo kiongozi wake ni Mitch McConnell kutoka chama cha Republican amesema zitawasilishwa siku ya Alhamisi mchana, zoezi litakalofuatiwa na kusikilizwa kesi siku ya Jumanne juma lijalo.

Trump amekuwa rais wa tatu katika historia ya Marekani kupigiwa kura ya matumizi mabaya ya madaraka

Kama Seneti haitapiga (uwezekano ni mkubwa) kura ya kumvua madaraka Trump,  ni nini maana ya mchakato wote huu?

 

Kama uliwasikiliza Democrats, sababu iliyowafanya wapitie yote haya hata kama mtazamo ni kwamba uwezekano wa Seneti (ambayo inatawaliwa na chama cha Trump cha Republican) wa kumpata na hatia ni mdogo sana au haupo ni kwa sababu wanahisi wanawajibu wa kumwajibisha rais kwa matendo yake.

 

Wanamtazama rais kama mtu aliyetumia vibaya mamlaka aliyonayo kuishinikiza Ukraine kuanzisha uchungzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa, na kama hawatachukua hatua, hata kama haitawezesha kuondolewa kwake madarakani , rais atalazimika kuchukua hatua zaidi ambazo zinaweza kuwa na athari kwa Democrat katika uchaguzi wa mwaka huu.

 

Halafu kuna ukweli halisi wa kisiasa kwamba makao makuu ya Democrat yamekuwa yakijiandaa kwa uchunguzi huu kwa miezi kadhaa.

 

Kama maafisa wakuu wa Democrat wasingelichukua hatua, wangekuwa katika hatari ya kuwakosa wafuasi wao au kukabiliwa na changamoto katika uchaguzi wa majimbo au kupoteza ufuasi katika uchaguzi mkuu kwa sababu wafuasi wao wasingehisi kuwa na msukumo wa kutosha wa kurejea katika uchaguzi.

Leave A Reply