The House of Favourite Newspapers

Bunge Lakabidhi Majoho kwa Makinda, Msekwa, Marehemu Sitta – Video

0

Mkutano wa 18 wa Bunge umeanza leo Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine Spika Ndugai amekabidhi majoho kwa Maspika Wastaafu waliowahi kuongoza Mhimili huo kwa nyakati tofauti kama ishara ya kutambua mchango wao kwenye utumishi uliotukuka Bungeni.


Maspika waliopewa heshima hiyo ni Spika Mstaafu Pius Msekwa, Marehemu Samuel Sitta ambaye amewakilishwa na Mkewe Mama Magreth Sitta na Anne Makinda.

 

Msekwa alikuwa Katibu wa Bunge wa kwanza Mtanzania na alihudumu katika nafasi ya Spika tangu Aprili 1994 hadi Novemba 2005.

 

Anne Makinda ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Spika hapa nchini ambapo alihudumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2010 hadi 2015.

Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta amepokea Joho alilokuwa akilifanyia kazi mumewe marehemu Samuel Sitta akiwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2010 hadi 2015 ikiwa ni kuenzi utendaji kazi wake. Margaret ametokwa machozi baada ya kupokea joho hilo.

 

Leave A Reply