The House of Favourite Newspapers

CLASS 2: Barnaba ‘Amenipiga’

0

MSANII chipukizi wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya Kidogo, Shedrack Allam ‘Class 2’ amedai kupigwa na msanii wa Bongo Fleva, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’.

 

Msanii huyo baada ya kufanya wimbo wake huo wa Kidogo aliomshirikisha Gabriel Gidabedi ‘G. Boy,’ alitaka kufanya kolabo ya wimbo wake mwingine unaoitwa Posa na Barnaba, hivyo akamuomba kaka wa msanii huyo, Omary Kamonalelo ‘Kamona,’ amsaidie kumpata ndipo alipojikuta akipigwa.

 

“Kaka yake aliniambia nitafute walau kiasi kadhaa cha pesa kama laki hivi ili Barnaba aweze kukubali kufanya kolabo na mimi. Nilipopata hiyo pesa nilimpa Barnaba pamoja na flash iliyokuwa na nyimbo mbili ambazo ni Kidogo ambao tayari ulikuwa umeshakamilika na ‘Posa’ ambao ndio nilitaka kufanya naye kolabo.

 

“Aliniambia nijitahidi nitoe video ili wimbo uwe na nguvu zaidi. Japo sina menejimenti, nilijitahidi nikatoa video yangu ambayo ilikuwa nzuri tu kisha nikaiwasilisha kwake.

 

“Baada ya hapo tulifanya makubaliano kuwa yeye atakuwa anachukua asilimia 10 ya kila kazi nitakayokuwa naitoa kwenye ukurasa wa YouTube kwa ajili ya kunisaidia kuzisukuma ngoma zangu. Nikamuongezea hela kama elfu hamsini, jumla ikawa laki na nusu kwa ajili ya hilo lakini baadaye akawa ananichenga tu,” alisema.

 

Alipotafutwa Barnaba kuhusu suala hilo, alimkana kuwa hamfahamu kabisa Shedrack wala hajawahi kufanya naye kazi.

 

“Mimi simjui kabisa Shedrack na wala hizo stori sizijui, kama yeye ananifahamu mimi simfahamu kabisa na sijawahi kufanya naye kazi.”

STORI: Irene Marango, Risasi.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by class2sonwise (@class2sonwise) on

Leave A Reply