The House of Favourite Newspapers

#CoronaVirus: Watanzania Wawili Watupwa Baharini

0

WATANZANIA wawili ambao majina yao ni Amiri Salamu (20) na Hassani Rajabu (30) walitoswa baharini na Wachina wakiwa wamepewa ‘life jackets’ na chupa za maji wakatakiwa kuogelea hadi nchi kavu Pwani ya jiji la Durban.

 

Nahodha wa meli ya mizigo ambaye ni raia wa China Cui Rongli amekiri kuwatupa Watanzania wawili baharini ambao walizamia katika meli hiyo akishirikiana na wenzake sita baada ya kuhofia kuwa wanaweza kuambukizwa virusi vya corona.

 

Amiri Salamu na Hassani Rajabu  walionusurika kifo baada ya kutupwa  sehemu yenye viumbe hatari wa majini katika Bahari ya Hindi eneo la Afrika Kusini. Watanzania hao walifanikiwa kuogelea kwa muda wa siku tatu ili kuokoa maisha yao hadi kufika katika ufukwe wa Zinkwazi karibu na mji wa Durban.

 

Wakala wa meli katika masuala ya usalama iliwatia nguvuni watuhumiwa hao baada ya meli yao ya MV TOP GRACE  kutia nanga katika bandari ya Richards Bay katika mji wa Kwazulu-Natal.

 

Nahodha amepigwa faini ya Dola 5,000 ambayo ni sawa na milioni 10 za Tanzania huku wafanyakazi wengine sita: Lin Xinyong, Zou Yongxian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun and Mu Yong, wakilipa kila mmoja faini ya Dola 2,500.

Leave A Reply