Dangote Wa Arusha Muuaji Watu, Watu Wajazana Na Mawe Mochwari – Video
Kijana mmoja wa Jijini Arusha maarufu kwa jina la Ally Dangote ambaye kwenye siku za karibuni amekuwa akisakwa hadi picha zake kubandikwa kwenye mitaa mbalimbali kutokana na tuhuma za kuchoma Watu 15 visu, kuua Watatu huku akiwa anavalia hijabu ili kujificha, amefariki dunia leo baada ya kudaiwa kujirusha kutoka kwenye gari la Polisi wakati akiwapeleka Polisi kwenda kuwafichua Wahalifu wenzake.
Mamia ya Watu walifurika nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mount Meru Arusha wakitaka kushuhudia kama ni kweli Kijana huyo amefariki kwani amekua tishio kwa Wakazi wengi hasa kutokana na mfululizo wa matukio yake ya kutisha ikiwemo kuwabaka Wanawake.