The House of Favourite Newspapers

Darasa si wa Mchezo, Tazma Alichokifanya

0

Albamu ya rapa Darassa a.k.a Mr Burudani, “Slave Becomes A King”, inaendelea kufanya vizuri duniani, ikiwa tayari ina miezi miwili pekee tangu iachiwe rasmi. Iliachiwa mwishoni mwa mwaka, na tayari imefikisha jumla ya streams MILIONI 138 kwenye majukwaa yote ya kusikiliza na kupakua muziki duniani (Digital Platforms).

 

 

“Slave Becomes A King” ina jumla ya nyimbo 21 alizowashirikisha wasanii tofauti tofauti kama #Alikiba, Marioo, Nandy, BillNass, ShoMadjozi na wengine wengi. Pia hii ndio album yake ya kwanza kwenye muziki wake.

 

 

Sanjali na hilo, Mr Burudani Darassa tayari kashaachia video mbili toka kwenye album hiyo, video hizo ni pamoja na Proud Of You (ft. AliKiba & Waiter) ukiacha ‘I Like It’ (ft. Sho Madjozi) ambayo ilitangulia mwaka jana.

Leave A Reply