DAS Mvomero Katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Akumbusha Kuienzi Misingi ya Umoja
Watanzania wamekumbushwa kuienzi misingi ya umoja wetu, mshikamano na udugu wetu kama Taifa Moja, kwani fahari hii tulioikuta sasa kuna Wazee wetu waliipigania mpaka sasa kuwa na Taifa lenye umoja, udugu, furaha na mshikamano.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero, Said Nguya katika maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliofanyika Chuo Kikuu Mzumbe.
Nguya amewataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea kwa kila mmoja kwa nafasi yake katika ujenzi wa Tanzania tunaitakayo kama njia ya kuwaenzi pia watangulizi wa taifa hili, na serikali kwa ujumla katika kuendelea kuiunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake.