The House of Favourite Newspapers

Diamond amlipua babaa’ke

0

DIAMOND (1)Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Musa Mateja
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amekata ukimya na kufungukia vilivyo ishu ya baba yake mzazi mzee Abdul kutamka kuwa siku akifa asitie mguu kwenye msiba hata kujipenyeza kwa namna yoyote akaligusa kaburi lake.

Baba Diamond aliitoa kauli hiyo hivi karibuni alipohojiwa na gazeti tumbo moja la hili la Ijumaa akimtuhumu mwanaye huyo kutomthamini hivyo haoni umuhimu wake.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia, Diamond amekuwa akiumizwa na kauli hiyo nzito aliyoitoa mzee Abdul wakati haoni sababu ya kuitamka wakati si kweli kwamba hamsaidii.

BABADBaba mzazi wa Diamond, mzee Abdul.

“Diamond amemaindi kweli. Anasema si kwamba hamsaidii, anampa fedha mara kwa mara. Anashindwa kuelewa lawama zinatoka wapi wakati yeye pamoja na ndugu zake kina Queen Darleen wanashirikiana kumsaidia.

“Yaani kiukweli Diamond imefika wakati anasema mzee atakuwa na kinyongo naye ambacho hakina sababu yoyote. Anahoji anataka amfanyie nini zaidi? Suala la kuishi naye haliwezekani sababu tangu akiwa mdogo, Diamond amezoea kulelewa na mama yake.

“Kama unavyojua mama na baba yake Diamond walishatengana, yeye kachagua kukaa na mama yake haiwezekani akaishi kwa baba yake, yeye atampa stahiki zote kama afanyavyo kila siku, inafika wakati hadi analazimika kutaka kutoa na yeye kauli mbaya, anashindwa sababu ana hofu ya Mungu,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilimsaka Diamond mwenyewe ambapo alisema anashangazwa na habari hizo kwani ukweli ni kwamba hana tatizo na mzazi wake hivyo suala la kusema wasizikane yeye halitambui kwani halina maana.

“Mimi sina tatizo na mzee wangu, maana nimekuwa nikimtimizia kila kinachohitajika sasa anasema tusizikane kwa lipi? Tatizo langu mimi nini? Si kweli kama mimi simsaidii. Huo ni uongo na sijui unatoka wapi.

Kama ni suala la kuishi mimi tangu zamani naishi na mama hivyo si rahisi kuhama sasa. Huo ndiyo msimamo wangu. Sina kinyongo naye na hata leo (Jumatano iliyopita) nimetoka kumtumia fedha ya sikukuu,” alisema Diamond.

Leave A Reply