The House of Favourite Newspapers

Funga Kazi: Jjiji Lazizima Tigo Wakitoa Milioni 5 Kwa Mshindi Wa “Cha Wote”- Mbagala

0
Meneja wa Kanda Bwn.  Jansen Msechu akizungumza kwenye hafla hiyo.

Bi Halima Rajabu Seleman, mfanyabiashara ndogondogo mkazi wa Kilungule – Mbagala Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni tano wa Kampeni ya Tigo CHA WOTE ambapo hadi sasa imebaki wiki moja tu Kutamatisha kampeni hii iliyowanufaisha wateja wengi Tigo wameshatoa fedha taslim na zawadi mbalimbali kwa washindi zaidi ya elfu 24 nchi nzima.
Akizungumza leo Septemba 8, 2023. Wakati wa Kumkabidhi mshindi Bi Halima mfano wa Hundi ya milioni tano maeneo ya Mbagala Zakhiem Jijini Dar Es Salaam, Meneja wa Kanda Bwn.  Jansen Msechu amesema kuwa hadi sasa ikiwa imebaki wiki moja kampeni Ya Cha Wote iishe wameshapatikana washindi zaidi ya elfu 24 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Bi Halima Rajabu Seleman (mwenye hijjab) akikabidhiwa mfano wa hundi ya fedha alizojishindia.

“Leo tunayo furaha kubwa kumkabidhi Bi Halima milioni tano yake, lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku.

Pamoja na zawadi za dakika na SMS kwa watumiaji wa Mtandao wa Tigo, kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu, Kununua Vifurushi, Kulipia Bili kwa Tigo Pesa, n.k.

Shamrashamra mitaani

Kwa kufanya hivyo na wewe siku si nyingi utakua miongoni mwa washindi wa kampeni hii ya CHA WOTE ndani ya hii wiki iliyobakia”. amesema Bwn Jensen.
Naye kwa Upande Wake Bi Halima mmoja wa washindi wa milioni tano, ameipongeza sana Kampuni ya Tigo kwa zawadi hii na kusema kuwa milioni tano, hii itamsaidia sana kuboresha biashara zake ndogondogo anazozifanya.
“Kwakweli asanteni sana Tigo na nawasihi watanzania wafanye miamala kwa wingi,  kununua vifurushi na Lipa kwa Simu maana ndio siri pekee ya Ushindi,” Alimalizia Bi. Halima.

Leave A Reply