Gazetia la ‘Ijumaa’ Laanza Kumwaga Zawadi kwa Wasomaji
GAZETI namba moja la habari za burudani na mastaa nchini la Ijumaa limekuja kivingine baada ya kuzindua promosheni yake mpya ya chemsha bongo ambayo itakuwa inawawezesha wasomaji kujinyakulia zawadi kibao ikiwemo mkwanja kila wiki.
Timu ya Masoko ya Global Publishers imetua mtaani leo na kuzindua rasmi promosheni hiyo ambapo msomaji atakayenunua gazeti hilo linalouzwa mtaani kwa Tsh 1,000 tu na kujibu maswali yaliyopo kwenye ukurasa wa pili, atakuwa ameingia katika kinyang’anyiro hicho cha ushindi.
Kampuni ya Global Group kazi yake ni kuhakikisha inawajali wasomaji wake kwa kuwarudishia fadhila, ndiyo maana imekuwa ikiwaletea zawadi mbalimbali kupitia promosheni mbalimbali na bahati nasibu.
Katika kuhakikisha chemsha bongo hiyo inawafikia wasomaji wake, timu ya maofisa masoko wa Global Publishers wameendelea kuwahamasisha wasomaji kununua nakala za gazeti hilo na kujibu maswali yanayopatikana katika ukurasa wa pili.
“Ukinunua Gazeti la Ijumaa ukurasa wa pili utakutana na chemsha bongo ambayo itakuwezesha kujibu maswali ili kujishindia Tsh. 30,000 (elfu thelathini) na tisheti bomba kabisa,” amesema Anthony Adam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wakati akiwaelezea wasomaji.
Baada ya kuhamishia mitandaoni pekee magazeti mengine ya Udaku ya Global Publishers, Ijumaa ndiyo Gazeti pekee la Burudani nchini Tanzania linalopatikana mtaani kwa sasa ambalo limeboreshwa kuanzia stori, upambaji wa kurasa, makala, machombezo na hadithi za mtunzi mahiri, Eric Shigongo.
Aidha, Ijumaa limesheheni kolamu zote kali zilizokuwa kwenye magazeti mengine Udaku ili kukufanya usi-miss kitu hata kimoja cha udaku iwe ndani ama nje ya Tanzania.
NA DENIS MTIMA | GPL