The House of Favourite Newspapers

GUU LA MAKAMBO LAMPOTEZA OKWI

Heritier Makambo wa Yanga.

 

MASTAA watano wanakimbizana na kuchuana vikali kwenye ishu ya ufungaji katika ligi ya msimu huu. Hao ni Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao nane, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere wa Simba wote wana saba sawa na Heritier Makambo wa Yanga na Said Dilunga wa Ruvu Shooting.

 

Lakini mjadala mkubwa wa mashabiki wa soka ni aina ya mabao waliyofunga Okwi, Makambo na Kagere ambao wote ni wachezaji wa kigeni wanaolipwa fedha nyingi. Kagere aliiambia Spoti Xtra kwamba hana presha na hali inayoendelea kwa vile anajua ishu kubwa anapaswa kutupia tu ili timu yake irudi kilele na yeye akae sawa. Tathmini ya mabao yao saba inaonyesha kwamba yale ya Makambo yana utofauti na wenzie.

MAKAMBO Ni raia wa DR Congo mwenye kasi ya kobe kwa kuwa anafunga bao moja katika mechi zake alizocheza lakini anawakaba vilivyo Okwi na Kagere. Katika mabao yake manne amefunga kwa mguu wa kushoto na matatu ni ya vichwa. Mabao yote kafunga kipindi cha kwanza. Inaonekana kwamba ukimdhidhibiti kipindi cha kwanza huenda akawa hana madhara. Mabao 6 amefunga ndani ya kumi na nane na bao moja nje ya boksi.

 

Pia katika mechi zote alizofunga mabao hayo, yeye ndiye anakuwa mchezaji wa kwanza kwenye mechi husika kuanza kucheka na nyavu. Hakuna mwingine aliyefanya hivyo. Mabao hayo alifunga katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar dakika ya 30. Coastal Union dakika ya 10, Lipuli dakika ya 9, JKT Tanzania dakika ya 17, Alliance FC dakika ya 22, Kagera Sugar dakika ya 22 na Mwadui dakika ya 10.

 

KAGERE Huyu ni Mnyarwanda, amefunga mabao 7. Kati ya hayo amefunga manne kwa mguu wa kulia na kufunga bao maoja kwa mguu wa kushoto na mabao maili kwa kichwa. Huyu ndiye mchezaji pekee ambaye ameweza kufunga kwa miguu yote lakini na kichwa. Mabao sita amefunga ndani ya 18 na moja akiwa nje ya 18. Katika

Emmanuel Okwi

kipindi cha kwanza ametupia mabao matano ikiwa ni katika dakika ya 2 dhidi ya Prisons, dakika ya 12 dhidi ya Mbeya City, dakika ya 18 na 38 dhidi ya JKT Tanzania, dakika ya 28 dhidi ya Ruvu Shooting kipindi cha pili alifunga dakika 49 dhidi ya Mbeya City na dakika ya 50 dhidi ya Mwadui.

 

OKWI Mashabiki wanasema ndiye straika mwenye Simba yake. Ni mfungaji bora wa msimu uliopita ana mabao saba kwenye ligi, mpaka sasa ambayo ameyafunga manne ametumia mguu wa kulia na kufunga matatu kwa kichwa. Ni bao moja tu katupia akiwa nje ya 18 na anatumia sana mguu wa kulia tofauti na wenzie Kagere na Makambo. Amefunga mabao manne kipindi cha pili na cha kwanza akitupia mabao matatu.

 

Cha kwanza alifunga dhidi ya Ruvu Shooting dakika ya 18, Alliance FC dakika ya 10 na Stand United dakika ya 45 na kipindi cha pili akifunga dhidi ya Ruvu Shooting dakika ya 52 na 77, African Lyon dakika ya 47 na Alliance dakika ya 62.

Simba waondoka kibabe usiku mnene kuifata mbabane swallows

Comments are closed.