The House of Favourite Newspapers

Haji Manara Amlilia Hans Pope

0

 

Nimechelewa sana kusikia taarifa za huu msiba wa mzee wetu Zacharia. Imenifadhaisha sana na imeniondolea Mood yangu. Kwangu alikuwa Mwanamichezo halisi shupavu na ameacha pengo kubwa Kwa mpira wetu na klabu yake Kwa ujumla. Pumzika Kwa amani Captain.

……………….

Picha ya kumbukumbu wakati wa Sikukuu ya Eid mwaka juzi ,familia hii ya Soka iliponitembela nyumbani kwangu. Marehemu Zacharia kushoto, Baba yangu Sunday Manara, Ceo wa Yanga Senzo ,Rais wa zamani wa Simba Evans Aveva,na mwisho kulia ni Mr Magori.

 

Mungu ndio anaemua nani atangulie. Pumzika Captain mstaafu 😭😭mtani na rafiki mkubwa wa watoto wako. Duniani tunapita tu.

…………………

Kutoka kwenye kinywa chake mwenyew nilimjua vema Captain kama nilivyopenda kumwita kwa jina hilo siku zote,,,
Licha ya kutembeleana mara kwa mara,,nimesafiri nae mara nyingi mno kwa gari yake kwenda mikoani kwenye mechi za Ligi.

 

Ni mjuzi wa hadithi za maisha na kiukweli alikuwa na hadithi nyingi tamu ,,moja ya hadithi tamu nnayoifikiria kuiandikia hata kitabu ni vita ya kagera ambayo Captain alipigana na ile sakata la kesi yao!!

 

Alinihadithia pia kuhusu jinsi yeye alivyofanikiwa kuwa Mfanyabiashara mkubwa baada ya miaka mingi ya kuishi Gerezani. Hakika Captain Zacharia alikuwa ni Chuo kamili kwa waliomfahamu na mjuzi wa dunia na ishtighali zake.

 

U know what. Licha ya kuwa Mkristo lakini anaweza kusoma Suraat Yaasin nzima bila kuangalia mahali. Usilolijua kuhusu yeye pia ni fundi wa kucharaza Gitaa la Solo na kwenye uvulana wake akiwa mdogo alishiriki kiasi na bendi ya Safari Trippers kama Mwanamuziki akiwa na Marehemu Marijani Rajabu.

Pumzika Father 😭😭😭

 

Leave A Reply