The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Mwili wa Hayati Magufuli Wawasili Kwao Chato – Video

0

HATIMAYE mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli umewasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Jumatano, Machi 24, 2021 majira ya saa 12:20 jioni ukitokea jijini Mwanza ambako umeagwa asubuhi ya leo na wakazi wa jiji hilo.

Safari ya kutoka jijini Mwanza imeanza majira ya saa 5:00 asubuhi baada ya kuagwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo mwili huo ulipitishwa katika kivuko cha Kigongo – Busisi (na kusimama kwa dakika chache ili ndugu na wazee wa eneo la nyumbani kwao na Mama Janeth Magufuli watoe heshima zao za mwisho) kisha mwili ulielekea Sengerema, Geita mjini mpaka Chato.

Maelfu ya wananchi wameonekana wakijipanga katika pande zote za barabara kuuaga mwili wa Hayati Magufuli huku wengine wakimwaga machozi ya huzuni na wengine wakiimba nyimbo mbalimbali za maombolezo na kumuaga kiongozi huyo wa Taifa la Tanzania.

Mwili wa Magufuli utaagwa kesho katika Uwanja wa Magufuli, Chato ambapo keshokutwa Machi 26, 2021, utazikwa katika eneo maalum lililoandaliwa hapohapo nyumbani kwake ambapo safari yake itahitimishwa hapo.

Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo yaliyokuwa aykimsumbua kwa miaka 10.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidhiwe.

Leave A Reply