The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Paula Aanza Masomo Uturuki

0

Baada ya kusemwa mambo mengi juu ya safari yake ya kwenda masomoni akidaiwa kuishia Dubai, hatimaye kitendawili kimeteguliwa baada ya kuanza masomo rasmi katika Chuo cha Maltepe University kilichopo katika Jiji la Istanbul nchini Uturuki.

Kabla ya kuanza masomo, Paula alipofika tu Dubai alipiga picha kwenye mgahawa maarufu jijini Istanbul na kuwaaminisha watu kweli yupo Uturuki.

Kupitia Insta Story yake, Paula ameweka video zikimuonesha akiwa chuoni hapo tayari kwa kuanza masomo huku akieleza kummisi mama yake, Kajala Masanja.

Juu ya kozi anayosomea, chuo hicho kina kozi nyingi kama uhandishi, famasi, mawasiliano, utengenezaji wa filamu, vipindi vya runinga na redio na nyingine nyingi.

Swali linaloulizwa na wengi ni kwamba, je, ataweza kusoma ilihali amemuacha mpenzi wake, Rayvanny nchini Tanzania?
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply