The House of Favourite Newspapers

Hotuba ya Kikwete, Mkapa, Wakiaga Mwili wa Moi – Video

0

Marais wastaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete baada ya kutua Jijini Nairobi kwa ajili ya mazishi rasmi ya Rais mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel arap Moi, walipata wasaa wakutoa salamu za rambimbali.

 

Rais Mstaafu Kikwete wakati akizungumza kutoa heshima za mwisho, kwa Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi, katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mjini Nairobi, alisema; “Tupo pamoja nanyi, niko pamoja nanyi, msiba wenu ni wangu, msiba wenu ni wetu, uchungu wenu ni wangu, uchungu wenu ni wetu, maombolezo yenu ni yangu na ni maombolezo yetu sisi wote”

 

“Nimejifunza mengi kutoka kwake (Moi), staili ya uongozi, namna ya kuhusiana na watu, namna ya kuheshimu watu, namna ya kupenda watu. Kwa hiyo ninaelewa kwa nini wakenya mnaomboleza na kusikitika sana kwa kifo chake,” alisema Rais Kikwete.

Naye Rais Mstaafu Mkapa alisema; ”Nilikuwa Rais wa Tanzania miaka kumi. Katika miaka hiyo kumi, miaka saba nilikuwa nafanya kazi na Rais Moi. Pamoja na kwamba ni mzee wetu, lakini kwangu mimi alikuwa ‘mentor’ wangu katika utawala na uongozi.

 

Ndio sababu nilisema lazima nije na ku ‘pay last tribute’ (kutoa heshima za mwisho) kwa uhusiano huo niliokuwa nao, lakini vilevile kushirikiana nanyi katika kumuombea, apumzike mahali pema peponi, kwa Mungu wetu ambaye alimpenda sana,” alisema Rais Mkapa.

Leave A Reply