The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Jay Z Alimzuia Kabisa Tiwa Savage Kufanya Hili… ( Video)

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuwa wasanii wengi wanaosign na label kubwa za Marekani mara nyingi huishia kupotea kwenye game, na Tiwa Savage ni miongoni mwa wasanii waliohofiwa kutokewa kwa jambo hilo baada ya kusign mkataba na Roc Nation label ya Jay Z.

Nimekutana na interview moja aliyofanya Tiwa Savage hivi karibuni na NotJustOK TV ya Nigeria. Ndani ya interview hiyo amezungumzia vitu vingi vya maisha yake ya sasa ikiwemo pia maisha yake ya kimuziki toka ajiunge Roc Nation. Moja ya vitu alivyoviweka sawa ni pamoja na kutuliza hofu za watu kuwa Roc Nation inamlazimisha kubadilisha aina ya muziki anaoufanya ambapo alisema:

Ninachokipenda kuhusu kukutana na kukaa na Jay Z ni alituambia mimi na Jazzy kuwa hataki nibadilike, alinizuia kabisa. Alisema kwa msisitizo kuwa kilichomvutia kuhusu mimi na brand yangu ni kile nilichokuwa nakifanya… “- Tiwa Savage.

Tiwa Savage pia alichukua time na kuweka sawa kuwa bado yupo Mavin Records na Don Jazzy:

Nimesigniwa Roc Nation, nina mkataba wa kuwa- managed huko lakini label niliyopo ambayo ni familia yangu bado ni Mavin Records… ” – alisema Tiwa Savage.

Hapo awali Don Jazzy aliwahi pia kufanya interview na NotJustOK TV na kufafanua mkataba wa Tiwa Savage na Roc Nation ambapo alisema:

Alichokisign Tiwa Savage na Roc Nation ni mkataba wa management na sio mkataba wa kurekodi muziki au album. Bado yupo Mavin Records ila Roc Nation inamsimamia kwa upande wa Management kwa kule. Unajua kuna milango ambayo Mavin Records inaweza kufungua lakini kuna milango ambayo hatuwezi kuifungua kwa nguvu zetu na hapo ndipo ambapo Roc Nation inaingia. Kazi yao ni kutusaidia kufungua milango mikubwa zaidi ambayo sisi hatuwezi kuifungua. Kwahiyo Roc Nation inasaidia kum-manage Tiwa Savage  kwa kule ila label aliyosainiwa ni Mavin Records. ” -Don Jazzy.

Itazame interview ya Tiwa Savage na NotJustOK TV ya Nigeira hapa chini.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.