JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA ZILIZOKUWA ZINATUMIWA NA WAHALIFU
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Liberates Sabas amesema Jeshi la Polisi kwa sasa linaendesha Operesheni mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Nchi ya Msumbiji ili kuwakabili wahalifu wanaokimbili nchini humu.
Aidha Jeshi la Polisi kupitia Operesheni Maalum inayoendelea mkoani Mtwara limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 96 kati yao 10 wamefikishwa mahakamani kwa kesi mbalimbali na wengine 16 wamefikishwa katika idara ya Uhamiaji kwa makosa yanayohusu maswala ya uhamiaji katika operesheni hiyo kumepatikana siraha mbili zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
Aidha Afande Sabas amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri ndani ya Jeshi la Polisi na kuwataka wananchi wote nchini kuendelea kutoa ushirikiano ili kutokomeza uhalifu nchini.
Comments are closed.