The House of Favourite Newspapers

Jide Afunguka: Sina Mpango wa Kufungua Record Label – Video

0

 

MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu ya Bongo Fleva, Lady Jay Dee, ametinga ndani ya studio za Global Radio kwenye kipindi ncha BONGO 255, na kufunguka ishu mbalimbali kuhusu muziki wake.

 

Jide ambaye Februari 12, 2021, anatarajia kuachia albamu yake mpya pale Serena Hotel inayokwenda kwa jina la 20, amesema: “Nimekuwa nikifanya vizuri na kazi zangu zinakubalika kwa sababu ya ‘consistence’ na ‘discipline’ kwenye kazi, naipenda sana kazi yangu ndiyo maana nafanya vizuri.

 

“Kazi zote ninazoletewa kwa ajili ya kushirikishwa ninazipenda kwa sababu kabla ya kushiriki katika kazi na msanii yeyote lazima niwe nimeisikiliza na nimeipenda ndipo nafanya maamuzi ya kushirikiana naye.

 

“Mambo yamebadilika, watu wengi wapo kwenye social media, mtu anaweza kuimba akaposti mitandaoni wakamuona, si lazima akashindane sehemu. Mimi nilimpata Rapcha kupitia Instagram, nilifanya shindano la rap, then Rapcha akashinda nikafanya chorus ya wimbo wake.

 

“Sijawahi kuwaza kuwa na record label kwa sababu si kila msanii lazima awe na record label, unaweza kumsaidia msanii hata kwa kufanya naye kolabo bila kumchaji chochote, hata kuwa role model wake ni msaada mkubwa kwake.

 

MSIKILIZE JIDE HAPA

Leave A Reply