The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya Kupika Kitoweo cha Kuku

0

 

KITOWEO cha kuku kinapendwa na watu wengi, leo nitaelezea mapishi tofauti ya kitoweo hicho.

MAHITAJI

Kuku mmoja wa 1

Vitunguu maji 3

NYANYA 5

Mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi kijiko 1 cha mezani

Mchanganyiko wa viungo/ garam masala/ mahanjumati masala vijiko 2 vya mezani

 

MAFUTA VIJIKO 4

Pilipili manga kijiko cha chai nusu

Bilinganya moja iwe teketeke Kijiko kimoja cha chai bizari ya njano. Chumvi kwa kiasi upendacho

Majani machache ya giligilani

JINSI YA KUPIKA Katakata kuku vipande vidogo vidogo kisha mchemshe – Inategemea aina ya kuku kama ni wa kisasa mchemshe kwa dakika 5; kama wa kienyeji ziwe dakika 15 – 20 .

Katika kumchemsha weka chumvi, majani ya giligilani na pilipili manga kidogo.

Baada ya kuku wako kuwa tayari – Chukua chombo utakachopikia weka mafuta acha yapate moto kiasi ndipo uweke vitunguu maji na viivishe dakika 2 ndipo uweke ule mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi na bilinganya kisha endelea kuivisha kwa dakika 3-5 ndipo uweke nyanya na ule mchanganyiko wa viungo au garam masala au mahanjumati masala, endelea kuivisha kama itaonekana kavu kabla ya kuiva ongeza ile supu uliyochemshia kuku. Kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.

Maoni ushauri +25578-8224474

Leave A Reply