The House of Favourite Newspapers

JPM: Wakikusumbua Sweka Ndani – Video

LEO Ijumaa, Novemba 22, 2019 Rais Dkt John Magufuli ameanzan ziara yake ya kikazi kwa siku Tano Jijini Dodoma ambapo ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru katika eneo la Maduka Chamwino.

 

“Nimefurahi mmenifikisha hapa kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, hizi fedha zimetoka siku nyingi lakini maendeleo ya kazi hayaridhishi.

 

“Kazi zimeanza,wananchi wa hapa Chamwino hasa vijana, nawaomba mshiriki kikamilifu, kwa wale mtakao pata nafasi ya kufanya kazi hapa, mshiriki kufanya hili jengo likamilike mapema, Mwezi wa nne kazi iwe imekamilika, jengo la ghorofa moja.

“Vya bure viliisha, vilimalizwa na Matonya sasa ni wakati wa kufanyakazi, mvua zimeanza kunyesha, limeni…heshima ya mji huu mtaileta kwa nyie kufanya kazi. Jeshi malizeni haraka jengo hili la Hospitali ya Uhuru hapa Dodoma, pesa zipo, timizeni wajibu wenu mmalize kazi,” amesema Magufuli.

 

Aidha, Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Soko Kuu Dodoma ambapo amependekeza liitwe Soko la Job Ndugai kama ishara ya kumuenzi spika katika jitahada zake kupitia

Bunge la Tanzania kutunga sheria ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya serikali. Mradi wa ujenzi wa soko hilo unagharimu Sh bilioni 14 na unatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2020.

 

Comments are closed.