The House of Favourite Newspapers

Katibu Mkuu Apata Ajali Akienda Maziko ya Moi

0

KATIBU Mkuu wa chama tawala nchini Kenya kiitwacho Jubilee, Raphael Tuju,  amepata ajali katika eneo la Magina, Barabara Kuu ya Nakuru-Nairobi.

 

Tuju alikuwa akielekea kwenye mazishi ya rais mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi,  eneo la Kabarak ambapo anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano, Februari 12, 2020.

Ripoti zinasema kuwa gari alimokua akisafiria liligongana na matatu na kupata majeraha madogo ingawa dereva wake amevunjika mkono katika ajali hiyo ya leo asubuhi.

 

Kamishna wa Kiambu Wilson Wanyaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema Tuju alikuwa katika gari aina ya Toyota Prado amepata majeraha kifuani na sehemu ya tumbo na kwamba yeye na dereva wake walipelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi.

 

Leave A Reply