The House of Favourite Newspapers

Katunzo: nitafanya mapinduzi bongo fleva

0

NA mwandishi wetu
MSANII anayetamba na wimbo wa Hunibanii, Mussa Katunzo amefunguka kuwa amedhamiria kufanya mapinduzi makubwa katika muziki wa Bongo Fleva kutokana na vitu alivyowekeza.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Katunzo ambaye wimbo huo unaopigwa katika vituo mbalimbali vya redio amemshirikisha staa wa Bongo Fleva, Herry Sameer ‘Mr Blue’, alisema amefungua studio kubwa ya sauti (audio) maeneo ya Sinza jijini Dar hivyo atakuwa na muda mzuri wa ngoma zake kuwa na ubora sambamba na za wasanii wengine.

“Ni studio kubwa na nzuri hivyo nitakuwa na muda mzuri wa kufanya nyimbo kali kwani ina vifaa vya kisasa ambavyo naamini muziki utakaozaliwa hapa ninaamini utaleta mapinduzi makubwa,” alisema Katunzo.

Leave A Reply