The House of Favourite Newspapers

Kiba Avunja Ukimywa Mbele ya JPM, Awaombea Pesa Bongo Movie – Video

0

MFALME wa Bongo Fleva, Alikiba ameiomba Serikali kutoa fedha ambazo zitasaidia wasanii hasa wa Bongo Movie kutengeneza filamu maalum itakayosaidia jamii kuelewa maisha aliyoyaishi hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

 

Kiba amesema hayo leo Jumatano, Oktoba 14, 2020 mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati aki-perform kwenye Jukwaa la Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

 

“Naomba sana itengwe bajeti maalumu kwa ajili ya wasanii wa filamu kutengeneza filamu itakayoelezea historia ya Baba wa ataifa ili vizazi vijavyo vijifunze kutokana na mazuri ya baba wa taifa,” amesema Msanii Alikiba.

Leave A Reply