The House of Favourite Newspapers

Kim, Kanye ‘Wamsapraiz’John Legend

0

Kutoka kushoto ni Kim Kardashian, Kanye West, John Legend na Chrissy Teigen.

WAFANANAO ndiyo wapendanao! Hili limedhihirishwa na mwanamitindo, Kim Kardashian na mumewe ambaye ni staa wa Hip Hop, Kanye West baada ya kuisapraiz familia ya John Legend ambaye ni staa wa Muziki wa R&B akiwa na mkewe ambaye ni mwanamitindo, Chrissy Teigen.

Kwa muda mrefu Chrissy amekuwa rafiki wa karibu na Kim Kardashian na urafiki wao ulianzia katika kazi ya mitindo. Hivi karibuni kupitia ukurasa wa Snapchat wa Chrissy alitupia picha ikimuonesha Kim akimbembeleza mtoto wake, Luna kisha akaandika;

“Shangazi!”

Siku hiyo, Kim, Kanye na mtoto wao, Saint West waliifanyia sapraiz familia hiyo kwa kujumuika pamoja katika Mgahawa wa Nobu huko Malibu.

Leave A Reply