The House of Favourite Newspapers

King Kiba Adaiwa Kuuza Silaha

0

MIONGONI mwa habari kubwa kwenye muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, ni tangazo la Mfalme Ali Saleh Kiba au King Kiba kutambilisha rasmi jina la albam yake iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake inayokwenda kwa jina la Only One King ambayo itatoka Oktoba 7, mwaka huu.

 

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake waliozungumza na Gazeti la IJUMAA wameonesha kuwa na shaka kwamba huwenda kwa kufanya hivyo atakuwa ameuza silaha kwa mahasimu wake kimuziki ambao nao wametangaza kuachia albam zao.

 

“Naamini kabisa kwa kufanya hivyo, Kiba atakuwa ameuza silaha kwa maadui zake ambao ni Diamond Platnumz na Harmonize au Konde Boy Mjeshi kwa sababu nao wametangaza kuachia albam zao.

 

“Sijajua kama amelifikiria hilo, lakini kila kitu kimeshakuwa wazi kuanzia ngoma zitakazokuwepo, kolabo zake hadi kava la albam, sasa kwa ninavyowajua upande wa pili (mahasimu), lazima watafanya jambo hapo katikati ili kumvurugia King Kiba.

 

“Wale wa upande wa pili tunawajua, walikuwa wanasikiliziana ni nani ataanza ili kujua ana silaha gani kwa hiyo kitendo cha King Kiba kuanza, basi utarajie kuona sarakasi nyingi sana,” anasema andrew_Kiba ambaye ni shabiki kindakindaki wa Kings Music.

 

King Kiba ambaye pia ni C.E.O wa Lebo ya Kings Music aliwaambia wanahabari juzi kuwa, sababu kuu iliyomsukuma kutoa albam hiyo ni malalamiko kutoka kwa mashabiki wake ambao walidai kuwa hafanyi kolabo kwa kiwango wanachokitaka.

 

“In general muziki wangu sijawa nikifanya collaboration, lakini nimeamua kufanya safari hii kwa kuwaonesha kwamba nimesikia kelele zao na kwa mapenzi na kuwaheshimisha,” anasema Kiba ambaye albam hiyo inakuja baada ya nyingine kama Cinderella na Ali K 4 Real.

STORI; RICHARD ITEMBE, TUDARCO

Leave A Reply