The House of Favourite Newspapers

Kubenea Aanika Mazito Asema ‘Bado Nipo Chadema’ – Video

0

 

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  amesema licha ya tetesi kusambaa kuwa anataka kukihama chama  chicho, amesisitiza hana mpango  huo hajaona sababu ya kufanya hivyo.

 

Amesema hayo leo Alhamisi, Aprili 2, 2020, alpozungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku nne tangu rafiki yake na Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema) kutangaza nia ya kukihama chama hicho na kujiunga NCCR -Mageuzi baada ya kumaliza ubunge wake mwaka huu.

 

“Baada ya Anthony Komu kutangaza kuondoka #Chadema yamekuwepo maneno mengi nikitajwa na mimi nitamfuata.  Komu ni ndugu yangu kabisa, lakini urafiki wetu haunifanyi kila anachofanya nami nikifanye, mimi bado ni mbunge wa #Chadema.

 

“Mimi nimeshaenda mahakamani mara nyingi sana, lakini inategemea na nafasi yangu na mimi naamini siyo lazima watu wote kukusanyika katika tukio moja, mimi nashiriki kwenye shughuli za Chadema, sina shida na chama na nipo pamoja na viongozi wangu.

 

“Nataka wananchi wenzangu wa Ubungo na Dar es Salaam pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi zinapaswa kuungwa mkono na jamii ili wananchi wajue madhara ya ugonjwa huu wa Corona, tufuate ushauri wa wataalam. Kuna hatari kubwa za kiafya kutoka nchi tajiri duniani juu ya gonjwa hili la Corona, sembuse sisi Tanzania? Mungu atunusuru na haya mambo ya kufanya mzaha.

 

“Nimshukuru Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kupunguza idadi ya wabunge Bungeni, ametumia mamlaka yake kwa mujibu wa katiba kulinda afya za wabunge lakini haitoshi, ni vizuri bunge likafungwa kama maambukizi yataendelea ili  kuokoa maisha ya watu.

 

“Tunatambua kuwa mapato ya serikali yanategemea kodi na mapato makubwa ni ya utalii, tutegemee uwepo wa mdororo wa uchumi duniani kwa sababu ya gonjwa hili la #corona.  Huu siyo wakati wa kurushiana vijembe na kuonyeshana ubabe, hii vita yetu sote, wakati wa vita ya Kagera, taifa lilikuwa pamoja, na huu ugonjwa ni lazima tushikamane pamoja kuhamasisha jamii ielimike na serikali isaidie.

 

“Inawezekana taarifa zinazotolewa sasa siyo za kweli kwa sababu kuna shida pia ya utambuzi ambayo ni jambo serious kabisa, tunaiomba serikali iwekeze katika maeneo ya kuhudumia wagonjwa.  Hili ni jambo jema, shule zilivyofungwa kwa sababu mzazi unakuwa karibu na mwanao, lakini kwa misongamano iliyopo kwenye madaladala unaona bora huyo mtoto angebaki shuleni.

 

Leave A Reply