The House of Favourite Newspapers

Kumwagana na Mpenzi Wake Eti ni Kiki


Nuh Mziwanda na Shilole wakiwa jukwaani

Na GLADNESS MALLYA |IJUMAA WIKIENDA| UBUYU ULIYONYOOKA

DAR ES SALAAM: Huu ubuyu si wa nchi hii! Habari za unyunyuzi zikufi kie kuwa, sakata la staa wa sinema na muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kumwagana na mpenzi wake, Boy Caro, limechukua sura mpya, ikisemekana kuwa eti ni kiki (ili wazungumzwe) kwani mwanamama huyo ana kitu anaandaa ambacho anataka kukibusti kwa njia hiyo.

Shilole katika Pozi.

MADAI YA KUMWAGANA

Hivi karibuni wawili hao walifunguka kwa nyakati tofauti wakikiri kwamba ni kweli wamemwagana huku kila mmoja akitoa sababu kuwa mwenzake hakuwa chaguo lake. Kufuatia ishu hiyo kuwa ndiyo habari ya mjini, Wikienda lilizama chimbo na kuibuka na Ubuyu Ulionyooka baada ya kunyetishiwa kutoka kwa rafiki wa karibu na mastaa hao ambaye alidai kuwa, Shilole na Boy Caro, waliamua kutoa kauli kuwa wameachana ikiwa ni muda mfupi tangu waingie kwenye uhusiano.

Nuh Mziwanda katika pozi

NUH ATAJWA

“Hivi mnajua kinachoendelea kati ya Shishi na Boy Caro? Sasa nawapa ubuyu wa ukweli kabisa kuwa watu hawa hawajaachana, wanatafuta kiki tu na wamekubaliana katika mpango huo wamuhusishe na Nuh Mziwanda (staa wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa) ndiyo maana unaona Shishi anamposti Nuh mara kwa mara kwenye ukurasa wake wa Instagram,” alimwaga ubuyu sosi huyo.

Nuh Mziwanda na Mkewe

MTU WA KARIBU

Baada ya kuzungumza  na sosi huyo, Wikienda lilizungumza na mtu mwingine wa karibu wa Shilole ambaye alidai kuwa, kuachana kwa wawili hao siyo kiki na sababu kubwa ni kuwa Shilole bado moyo wake uko kwa Nuh. “Kiukweli moyo wa Shishi bado upo kwa Nuh. Hata akienda kwa mwanaume gani, anajikuta amemrudia, hiyo ndiyo sababu kubwa ya mpenzi wake kushindwa na kuamua kuachana naye,” alisema rafi ki huyo wa Shishi.

SHILOLE AFUNGUKA

Shilole akiwa jukwaani

Baada ya kunyetishiwa ishu nzima na wadau hao wakubwa wa ubuyu, Wikienda lilimwendea hewani Shilole aliyekiri kuachana na mpenzi wakehuyo, lakini alipozidi kubanwa maswali, alikataa kujibu. “Yah tumeachana kweli kwa sababu nimegundua kuwa ana tabia ambazo haziendani na zangu,” alisema Shilole. Wikienda lilimbana Shilole juu ya madai ya kurudiana na Nuh na kwamba ndiyo sababu ya kumwagana na Boy Caro ambapo alidai kuwa hakuna kitu kama hicho na kwamba yeye ameamua kuachana na jamaa huyo kwa madai hayo aliyoyataja.

BOY CARO NAYE

Wikienda lilipomgeukia Boy Caro na kumuuliza kulikoni juu ya uhusiano wake na Shilole, alifunguka: “Kweli nimeachana na Shilole lakini siwezi kuweka wazi sababu za kuachana naye ila namsifu sana. Shilole ni mwanamke mpiganaji sana katika kutafuta maisha, lakini tumeshindwana, naomba niseme hivyo tu. Sababu za kuachana aulizwe yeye.”

HUYU HAPA NUH

Kwa upande wa Nuh alipoulizwa na Wikienda juu ya madai ya kuvunja penzi la Shilole na Boy Caro huku akiwasiliana na mrembo huyo kwa ujumbe mtamumtamu hasa usiku mnene, jamaa huyo alikuwa na haya ya kusema: “Sina uhusiano na Shishi Baby, yule ni mshkaji wangu tu, hakuna kitu kama hicho. Ukaribu wetu upo kwenye kazi tu.”

NENO LA MHARIRI

Labda kama ni kiki, lakini kiukweli Shilole sasa inabidi ajitathmini juu ya wanaume anaokuwanao kisha kumwagana bila utaratibu kwa sababu kwa kufanya hivyo anawajengea wanaye picha mbaya kwenye jamii.

Comments are closed.