The House of Favourite Newspapers

Lava Lava Afunguka Siri Nzito, Atamani Kuacha Muziki

0

MSANII wa Bongo Fleva, kutoka Lebo wa WCB, Lava Lava ameamua kuanika siri nzito iliyokuwa moyoni mwake huku akifunguka makubwa kuhusu alivyotamani kuacha muziki kutokana na mambo mengi mazito aliyoyapitia maishani.

 

Lava Lava amekuwa akitajwa kuwa hafanyi vizuri kwenye tasnia ya mzuiki ikilinganishwa na wasanii wengine wa lebo hiyo kama Rayvanny na Zuchu.

Kupitia akaunti yake, Lava Lava ameandika….

 

Leo naomba niwape story kwa kifupi juu ya hii project ya wimbo wa #Wanga: Mwanzoni wa huu mwaka wa 2020 kwa upande wangu haukuwa mzuri sana yani kuna mazingira nilikuwa napitia kibinadamu mpaka nikahisi sio kawaida.

 

Najua wengi watakuwa wamenielewa nini namaanisha, kiufupi nilikuwa na mawazo sana mpaka kufikia wakati nilitamani kabisa niache hata muziki wenyewe.

 

Ndipo nilikutana na mdogo wangu Meja Kunta; kwa mara ya kwanza na kutana naye pia alikuwa ana mawazo sana kuhusu ile skendo yake ya kifo, alichanganyikiwa kiukweli naye hakujua aanzie wapi na wala hajui hilo suala lilikuwa vipi na ataeleza nini kwa wananchi akingali bado mzima.

 

Katika maongezi  yetu tukawaza kwa nini sisi kama wasanii tusifanye kitu ambacho kitawasilisha hisia zetu kwa muda ule au mawazo yetu, basi tukaamua kwenda studio muda uleule.

 

Kabla hatujakwenda studio swali likaja tunaanzia wapi au tunafanya wimbo wa aina gani mana kama unavyojua Meja Kunta ni muimbaji wa singeli na mimi sijawahi kuimba singeli ila niliamini hakuna kitu kitashindikana japo meja alikuwa ana wasiwasi sana na uongozi wake.

 

Labda pengine sitoweza, huwezi amini niliuambia uongozi wa meja kuwa nimepata aidia ya wanga yaani/wachawi kutokana na mazingira tunayopitia itafaa sana.

 

Na kwa hapa nitoe pongezi kwa mama angu mzazi, kiukweli nilimpgia simu nikamuuliza nataka kuimba singeli na sijawahi kuimba nina aidia ya Wanga nifanyaje.

 

Akaniambia ‘kuna sound za nyimbo flani za kizamani kama zile segere zile yaani yale mavanga tumieni nahisi itafaa sana kwa mnachotaka kufanya.

 

Kweli akanitumia link tofauti tofauti tukapata moja tukaingia studio kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba wimbo wa Wanga kwanza ni hisia za kweli kabisa, cha pili tulirekodi siku moja tu ukamalizika kila kitu, na kesho yake ukatoka.

 

Hapa naomba management yangu itanisamehe maana hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua yaani sikutoa taarifa kwa kiongozi yoyote hata Diamond 💎 walishtukia tu wimbo uko YouTube.

 

Kitu nilichojifunza hapa kwanza, tusikate tamaa hata kama unapitia magumu kiasi gani (pambana), cha pili kitu ukikipenda na ukakifanya toka moyoni watu watakipenda tu, muziki naupenda na nina imani kuna siku nitafika ninapopataka, Mungu yupo mwenda pole hajikwai, wakati wa Mungu ni sahihi kuliko wa mwanadamu🙏🏼

Leave A Reply