JPM Afanya Maamuzi Mazito kwa Nape – Video

Rais Dkt. John Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama na ihamishiwe eneo la Mtama (ambalo ni Jimbo la Mbunge wa CCM, Nape Nnauye) kutoka kwenye jengo lililopo Lindi Mjini.

 

Amesema, ndani ya siku 15, Viongozi wa Halmashauri hiyo watoke Mjini na kuhamia Mtama na hiyo ndio italeta maendeleo kwani kama ni giza ndio watashughulikia umeme haraka.

 

“Najua kulikuwa na mabishano, wapo wanaotaka Makao Makuu yaende Subi, wapo waliotaka yaende Mchinga, wapo waliotaka yaende Rondo, kila mmoja alitaka. Kwa kuwa mimi ndio Rais, na mimi napasua katikati kwa kufuata haki, nimetoa maagizo, Manispaa ya Lindi itachukua eneo lake iliyokuwa nalo mpaka Mnazi Mmoja hadi Mingoyo na kuongezewa eneo la Mchinga.

 

“Niwapongeze kwa kupata Hospitali ya Wilaya hapa. Tumeipa Tsh Bil 1.5. Mkurungenzi na DC simamieni hospitali ikamilike. Pamekuwepo na mchezo wa watu kujilipa fedha za wananchi, Hospitali ya Mkoa ‘Sokoine’ pana upotevu wa fedha Tsh Mil. 86 zilizolipwa NHIF Lindi tangu Juni 2018 kutoka akaunti ya RAS, nataka hizi fedha zirudi, kuna gari aina ya Land Cruser Donor Funded Project namba 6794 la hospitali gari liliuzwa kwa Mhasibu Mkuu.

 

“Ninashukuru sana kwa kura nyingi mlizonipa pamoja na kijana wangu Nnauye Nape nawashukuru mno na nilivyokuwa naomba kura mlikuwepo wananchi wa Kiwalala na kura mkanipa nyingi. Mheshimiwa Mbunge a hapa (Nape Nnauye) ameeleza juu ya hatua mbalimbali tunazochukua ikiwa ni npamoja na kupeleka umeme vijijini tunataka ikifika 2021/22 vijiji vyote viwe vimepata umeme, pia tunashughulikia suala la maji,” amesema Rais Magufuli.

 

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemweleza Rais Magufuli kuwa Wizara yake imeshamaliza kuhakiki akaunti za benki za wakulima wa korosho wanaoidai Serikali na kufikia Jumanne ya wiki ijayo wakulima wote wa korosho Halmashauri ya Mtama watakuwa wamepata fedha zao.

RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA

 


Loading...

Toa comment