The House of Favourite Newspapers

Lucy Komba Amburuza Kortini Mdogo wa Mbasha

0
Mwigizaji wa Bongo Muvi, Lucy Komba.

NA MAYASA MARIWATA |  IJUMAA | HABARI

MWIGIZAJI wa Bongo Muvi, Lucy Komba amemburuza kortini mzazi mwenziye, Patrick Zulig Mbasha ambaye ni mdogo wa staa wa Gospo, Emmanuel Mbasha kwa madai kuwa amemtelekeza mwanaye Strom tangu azaliwe.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na Lucy ambaye amehamishia makazi yake nchini Denmark kwa mumewe, bishosti huyo aliamua kumshitaki Patrick kwa sababu alichukizwa na tabia ya kutompa matunzo ya mtoto wao waliyezaa miaka kadhaa iliyopita.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa, kila anapoitwa kwenye kesi hiyo, Patrick amekuwa hatii wito wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ambako ndiko ilikofunguliwa kesi hiyo.
Kufuatia ishu hiyo, Ijumaa liliwasiliana na Lucy ambaye alikiri kuwepo kwa kesi hiyo: “Ni kweli nimemshitaki Patrick ila kwa sasa mimi siyo mzungumzaji maana ni mambo ya kimahakama.” Kwa upande mwanaume huyo simu yake haikuwa hewani, alipotafutwa kaka yake, Emmanuel Mbasha alisema kuwa hafahamu chochote kuhusiana na kesi hiyo.

Leave A Reply