Lulu Diva Siwezi Kutoka na Vijana Marioo

Sexy lady kunako Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’, ameweka wazi kuwa anapenda sana hela na hivyo hawezi kutoka na mwanaume sharobaro asiyekuwa na hela.

 

Akipiga stori na Risasi Vibe Lulu amesema kuwa katika amishja yake, hawezi kutoka na vijana wadogo bali wazee maana vijana ni pasua kichwa wanategemea kulelewa tu.

 

“Mi napenda sana hela, hivyo siwezi kutoka na mwanaume ambaye hanipi hela, kwa maana mimi mzuri, mapenzi ni hela asikwambie mtu, hao marioo wanapenda kulelewa wanunuliwe hadi nguo, kwanza ni pasua kichwa kabisa na napenda kutoka na mwanaume aliyenizidi umri kama Baba yangu,’’ alisema Lulu Diva.

Stori: Happyness Masunga

Toa comment