The House of Favourite Newspapers

Makambo Aweka Rekodi ya Kibabe

Heritier Makambo

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kuweka rekodi ya aina yake baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo.

 

Makambo amefanya hivyo mfululizo ikiwa ni baada ya kupokea tuzo hiyo mara ya kwanza mwezi Novemba akiwashinda wachezaji wawili aliofika nao fainali Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki wa Yanga Abdalah Shaibu ‘Ninja’.

 

Mwezi Desemba amewashinda Miraj Athumani wa Lipuli na Idd Seleman ‘Nando’ wa Mbeya City.

Rekodi yake inakuwa ya kwanza kwani mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye ametwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo, Makambo anakunja shilingi milioni mbili mfukoni ambazo ni zawadi alizopewa baada ya kushinda tuzo hizo.

 

Mshindi wa kwanza alikuwa ni Meddie Kagere mwezi Agosti akafuatia Eliud Ambokile mwezi Septemba, Emanuel Okwi mwezi Oktoba, Novemba na Desemba zote akakomba Makambo tuzo pamoja na kisimbusi cha Azam TV.

 

Kwa upande wa Kocha, Mwinyi Zahera amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara tatu mpaka sasa ikiwa ni mwezi Septemba, Novemba na Desemba akiwaacha mbali makocha wengine wote wa kibongo huku Patrick Aussems akiishia kuingia fainali.

Comments are closed.