The House of Favourite Newspapers

Manara: Yanga Wananiogopa Wanatamani Nife!

0

MSEMAJI wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema mashabiki wa Yanga wanamwgopa sana, wanatetemeka na wengine wanatamani hadi afe pale wamwonapo ila ndiyo hivyo hawana cha kumfanya.

Manara amesema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga kumsema kwamba anaropoka sana.

 

“Nitajie neno moja ambalo unaona nimeropoka, baadhi ya mashabiki wa Yanga ndiyo wanasema naropoka sio watu, tena wanaotoka mitandaoni wapuuzi wanasema mimi naropoka sasa si ningekamatwa na polisi yaani niropoke halafu Serikali iniache, Yanga huwa wanajiona wakubwa na hawaguswi wanataka wawatanie Simba halafu wao wasitaniwe,” amesema.

 

Ameongeza kuwa; “Vyote ninavyoongea nina uhakika navyo hakuna hata kimoja nisichokuwa na uhakika, tangu nimeanza kuwa boksi Yanga wananiogopa halafu hawana cha kunifanya hata nikitokea wanatetemeka na wengine wanatamani nife”.

 

Kesho, Januari 4, 2020, kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu kati ya timu yake ya Simba dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, utakaochezwa majira ya saa 11:00 jioni, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Leave A Reply