The House of Favourite Newspapers

Mapokezi ya Magufuli Zanzibar ni Balaa! – Video

0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la (ATCL) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Marehemu Abeid Amani Karume jijini Zanzibar leo Ijumaa Oktoba 02.2020 tayari kwa mkutano wake wa kampeni utakaofanyika kesho kwenye viwanja ya Maisara jijini Zanzibar.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe ameshawasili Zanzibar leo, Ijumaa, Oktoba 2, 2020 akitokea Songwe na amepokelewa kwa nderemo na shangwe na wanachama wa CCM Visiwani humo.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya asili ya Zanzibar mara baada ya kushuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la ATCL wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Marehemu Abeid Amani Karume jijini Zanzibar leo Ijumaa Oktoba 02.2020 tayari kwa mkutano wake wa kampeni utakaofanyika kesho kwenye viwanja ya Maisara jijini Zanzibar.

Dkt. Magufuli amewasili Zanzinar kwa Ndege ya Watanzania Airbus (Twiga).

Kesho Oktoba 3, 2020 katika Viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar, Dkt. Magufuli atafanya Mkutano mkubwa wa Kampeni zake pamoja na kumuombea kura mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akikitunza kikundi cha ngoma kilichotumbuiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume jijini Zanzibar leo Ijumaa Oktoba 02.2020

 

 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akipungia mkono kukundi cha burudani kilichotumbuiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume jijini Zanzibar leo Ijumaa Oktoba 02.2020, Kulia ni Abdula Juma Sadala “Mabodi” Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar akipiga makofi.

 

Msanii wa Muziki wa kizazi Kipya Diamondplatnamz ni miongozi mwa wanamuziki walioongozana na mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipowasili jijini Zanzibar leo kushoto ni DJ Maarufu wa Diamondplatnamz Rommy Jons.

 

Leave A Reply