The House of Favourite Newspapers

Mary Mawigi Alia na Wanasiasa

Mary Mawigi.

Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| RISASI VIBES

MSANII wa filamu Bongo, Mary Mawigi amelia na wanasiasa, akiwataka kuangalia matatizo ya wananchi na kuyafanyia kazi, badala ya kuendekeza mambo ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

…akiwa na Lemutuz

Akipiga stori na Za Motomoto News, Mary alisema kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa, yupo njia panda kwani wanasiasa wamekuwa wakitafuta umaarufu mitandaoni badala ya kushughulika na matatizo yanayowakumba wananchi jambo ambalo linaumiza kwani walichaguliwa ili wawasaidie na kutetea haki zao, lakini wanaenda kinyume.

“Kiukweli inauma sana kuona wanasiasa wakilumbana kwa kitu kidogo na kusahau majukumu yao, tunaona watu wanapoteza maisha hospitalini kwa kukosa dawa na mahitaji mengine, lakini watu hawana habari, ndiyo maana sipendi siasa kabisa,” alisema Mary.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.