The House of Favourite Newspapers

MBATIA: JPM ONGEZA MISHAHARA YA WALIMU, KESHO MEI MOSI – VIDEO

AKICHANGIA mchango katika mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mbunge wa Vunjo (NCCR Mageuzi) James Mbatiaa ameishauri Serikali kuwajali walimu kwa kuwaongezea maslahi ya yao ikiwemo mishahara yao kwani ndiyo walezi wakuu wa watoto wa Taifa la Tanzania.

 

Mbatia amesema anashangazwa kuona Serikali haijali maslahi ya walimu wakati zaidi ya theruthi moja ya watumishi ni walimu. Ametoa ushauri kwa Serikali kuwajali sana walimu na hata kubadili msemo wa nani kama mama anataka uwe nani kama mwalimu.

 

Ametoa rai kwa Rais Dkt John Magufuli kesho wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi (Sikukuu ya Wafanyakazi) aongeze mishahara ya walimu ili kurudisha hali ya kufundisha kwa walimu wetu.

RAIS KESHO MEI MOSI ONGEZA MISHAHARA YA WALIMU -JAMES MBATIA

Comments are closed.