The House of Favourite Newspapers

Nyumba za Mbowe Zapekuliwa, Aachiwa Usiku wa Manane

DAR ES SALAAM: Jana  mchana Jumatatu Feb. 20, 2017, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi wakati akienda kujisalimisha, alipofikishwa kituoni alihojiwa na polisi kuhusu sakata la dawa za kulevya baada ya jina lake kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  February 8.

Baada ya kukaa kituoni hapo kwa zaidi ya saa mbili, Mwenyekiti huyo akichukuliwa na Gari aina ya Land Cruiser iliyofatwa na magari mengine nyuma yake na kuelekea nyumbani kwake.

Baadaye Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene alisema  Polisi walienda na Mbowe kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo alisema kwenye mida ya saa 6 usiku wa kuamkia leo Polisi walimrudisha Mbowe kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar, na wakamfungulia jalada la Uchunguzi.

Adidha kwa taarifa zilizotufikia leo asubuhi zimeeleza kuwa, Freeman Mbowe ameachiwa saa saba na robo usiku wa kuamkia leo baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi.

Tumaini Makene ameithibitisha taarifa za kuachiwa mwanasiasa huyo kuwa ni za kweli. Hata hivyo, taarifa iliyosambazwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu kupitia mitandao ya kijamii imesema kuwa chama hicho kitatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo leo.

“Tunawashukuru wote kwa sala, maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama saa kumi za mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam,” Mwalimu amesema.

Comments are closed.